"NIA YANGU NI KUIFANYA TANZANIA GHALA LA CHAKULA"
Fredric Karia ni Mkulima. Anafanya kilimo
cha nyanya, mpunga na mahindi. Mbali na kufamya kilimo pia ni Mukurugenzi wa
kampuni binasfi Kicharugu Logistic Limited. Fredrick ni mtaamu wa mambo ya
usalama wa majini na mazingira (Maritarime Safety and Environment Management)
Swali: Nini kilikusukuma ukaamua kufanya
kilimo?
Fredrick: Kwanza nilikataa kuwa maskini, nilifanya kila
njia kutimiza malengo yangu.
Wazo la
Kulisha Tanzania nzima, sikuona sababu ya
watu wa nje kuja nchini kutusaidia
wakati tuna ardhi nzuri na yenye rutuba. Nia yangu ni kuifanya Tanzania
ghala kuu la chakula, akitokea mtu mwingine mwenye mawazo kama yangu basi
Tanzania ile dhana ya “Kilimo Kwanza” itakua kweli
Fredrick: nilianza kulima si muda mrefu, ni
mwaka jana 2013 hadi sasa.
Nalima Mpunga na nyanya
Swali: ni mafanikio yapi uliyoyapata
kutokana na kilimo?
Mafanikio yapo. Nina eneo (ardhi) hekari
35 Dar es Salaam, hekari 3.5 Dododma, 3.5 Mlandizi na Kiluvya.
Pia nimewekeza kwenye viwanja
Swali: Unawezaje kufanya shuguri za
kilimo wakati muda mwingi unakua safarini au kwenye majukumu mengine?
Rafiki wa Fredrick, akiandaa shamba |
"Nikiwepo hua nafanya mwenyewe ila
ninaposafari wanakuwepo wafanyakazi wangu wa shamba. Kwa mfano sasa hivi sipo
nchini shughuri za shamba zipo chini ya rafiki yangu. Huwa namkabidhi vitu
vyote na mahitaji yote"
Shughuri zangu za shamba zinakwenda vizuri na mambo yote yapo kwenye taratibu nzuri ili kuhakikisha kilimo kinakua.
Swali: Changamoto zipi unakumbana nazo?
Zipo changamoto nyingi kwa kweli unaweza ukalima mwisho wa msimu ukitarajia kupata gunia 100
ukaanguka, na umetumia pesa nyingi tayari, pesa ikiwa ya mkopo ndio hasara
zaidi.
"Pia changamoto niliyonayo trekta la kukodi, "natumia gharama kubwa sana"
Changamoto nyingine ni wadudu wakishambulia mazao wanasababisha hasara kubwa hivyo umakini unahitajika hasa katika kufata taratibu za "kilimo cha kisasa"
Naungana na ANSAF kwenye kapeni ya "KILIMO INALIPA, JIKITE" kuwakumbusha viongozi wa Afrika kutenga asilimia 10 ya bajeti kwenye kilimo ili kuleta uzalishaji wenye tija.
Niliamua kulima mpunga baada ya kuona mchele ukitumika sana kwa chakula kwa watanzania walio wengi.
Napenda kuwaambia vijana wenzangu wasitegemee kuajiriwa peke yake kwani wanaweza kujiajiri wenyewe kupitia sekta hii ya kilimo.
ANSAF kupitia kapeni ya Kilimo Inalipa Jikite ina lengo la kuwasaidia wakulima wadogo ili kuondokana na lindi la umaskini.