Thursday 3 April 2014

FREDRICK KARIA: NINA NDOTO ZA KULISHA TANZANIA NZIMA


"NIA YANGU NI KUIFANYA TANZANIA GHALA LA CHAKULA"


Fredric Karia ni Mkulima. Anafanya kilimo cha nyanya, mpunga na mahindi. Mbali na kufamya kilimo pia ni Mukurugenzi wa kampuni binasfi Kicharugu Logistic Limited. Fredrick ni mtaamu wa mambo ya usalama wa majini na mazingira (Maritarime Safety and Environment Management)

Swali: Nini kilikusukuma ukaamua kufanya kilimo?

Fredrick:  Kwanza nilikataa kuwa maskini, nilifanya kila njia kutimiza malengo yangu.  
Wazo la Kulisha Tanzania nzima, sikuona sababu ya  watu wa nje kuja nchini kutusaidia  wakati tuna ardhi nzuri na yenye rutuba. Nia yangu ni kuifanya Tanzania ghala kuu la chakula, akitokea mtu mwingine mwenye mawazo kama yangu basi Tanzania ile dhana ya “Kilimo Kwanza” itakua kweli


Fredrick: nilianza kulima si muda mrefu, ni mwaka jana 2013 hadi sasa. 
Nalima Mpunga na nyanya

Swali: ni mafanikio yapi uliyoyapata kutokana na kilimo?



Mafanikio yapo. Nina eneo (ardhi) hekari 35 Dar es Salaam, hekari 3.5 Dododma, 3.5 Mlandizi  na Kiluvya. 
Pia nimewekeza kwenye viwanja








Swali: Unawezaje kufanya shuguri za kilimo wakati muda mwingi unakua safarini au kwenye majukumu mengine?

Rafiki wa Fredrick, akiandaa shamba


"Nikiwepo hua nafanya mwenyewe ila ninaposafari wanakuwepo wafanyakazi wangu wa shamba. Kwa mfano sasa hivi sipo nchini shughuri za shamba zipo chini ya rafiki yangu. Huwa namkabidhi vitu vyote na mahitaji yote"

Shughuri zangu za shamba zinakwenda vizuri na mambo yote yapo kwenye taratibu nzuri ili kuhakikisha kilimo kinakua. 







Swali: Changamoto zipi unakumbana nazo?



Zipo changamoto nyingi kwa kweli unaweza ukalima mwisho wa msimu ukitarajia kupata gunia 100 ukaanguka, na umetumia pesa nyingi tayari, pesa ikiwa ya mkopo ndio hasara zaidi.

  







"Pia changamoto niliyonayo trekta la kukodi, "natumia gharama kubwa sana" 

Changamoto nyingine ni wadudu wakishambulia mazao wanasababisha hasara kubwa hivyo umakini unahitajika hasa katika kufata taratibu za "kilimo cha kisasa"




Naungana na ANSAF kwenye kapeni ya "KILIMO INALIPA, JIKITE" kuwakumbusha viongozi wa Afrika kutenga asilimia 10 ya bajeti kwenye kilimo ili kuleta uzalishaji wenye tija.



Niliamua kulima mpunga baada ya kuona mchele ukitumika sana kwa chakula kwa watanzania walio wengi.

Napenda kuwaambia vijana wenzangu wasitegemee kuajiriwa peke yake kwani wanaweza kujiajiri wenyewe kupitia sekta hii ya kilimo.

ANSAF kupitia kapeni ya Kilimo Inalipa Jikite ina lengo la kuwasaidia wakulima wadogo ili kuondokana na lindi la umaskini.

Friday 21 March 2014

Masoud Kipanya:HAKUNA BIASHARA KUBWA ZAIDI YA KUZALISHA CHAKULA



 UKIWA MKULIMA UNAUWEZO WA KULISHA NA KUWA TAJIRI

 Masoud Kipanya akizungumza na wakulima


Mercy, Mwakilishi kutoka Shirika la ONE katika mazungumzo yake alisema kwamba tajiri mkubwa wa afrika anaitwa Dangote ni mkulima, maana yake nini? 

Maana yake Dangote sio kwamba analima hewani ila anafanya taratibu zote kama sisi tunavyofanya.  Yeye anaishi Nijeria, ardhi iliyopo huko ni sawa na iliyopo Tanzania tena inawezekana Tanzania ikawa na maeneo mazuri zaidi. 

Sisi kama binaadamu tunaweza kua mabilioni, kwa sababu binaadamu anaweza kuacha vitu vyote lakini chakula ni lazima ale, sasa kuna biashara kubwa zaidi ya kuzalisha chakula? Hakuna.
Ukiwa mkulima unanfasi kubwa ya kulisha jamii lakini vile vile na kutajirika. 
 Kipanya akisisitiza umuhimu wa kilimo

Mimi kama Masoud Kipanya nina miradi miwili ambayo ninaifanya.Wa kwanza ni Maisha plus-kipindi cha televishen sasa hivi tunawaganisha vijana pamoja na wakina mama wazalishaji wa chakula. Nia yetu kubwa ni kuwaambukiza hawa vijana ili hii tabia ya kutoroka kutoka vijijini kukimbilia mijini iweze kuisha, watu waweze kujua namna wanavyoweza kutembea juu ya hela wakiwa kijijini .

Mradi wa pili tunaufanya na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, ambapo tuna vijana 100 tumewaweka porini kwa kufuata model ileile ya maisha plus. Wale vijana 100 tumeanza kukaa nao tangu mwaka jana (2013) mwezi 4 na wanafanya kilimo cha hali ya juu kabisa. Hata mimi mwenyewe mjini nimeanza kuhama kabisa utanikiuta Tabora. Dar es salam tunaacha AC, magari mazuri kwa sababu tunajua tunakoelekea.


Mwaka huu vijana wamelima hekta 20 za tumbaku lakini vile vile wanalima na mahindi. Mwakani wanatarajia kulima hekta 100 kwa hivyo kuna unawezekano wa kutengeneza milioni 700 au 800 ni mkubwa sana. Sasa unasemaje kuhusu kilimo?

Masoud Kipanya akiwa na mabalozi wenzake, Profesa J na Mrisho Mpoto











Thursday 20 March 2014

Joseph Haule: Dhamira yetu ni kufanya Tanzania iweze kupata Maendeleo kupitia Kilimo

SOTE TUNAAMINI KILIMO NDIO UTI WA MGONGO WA TAIFA LETU!

 Profesa J, ambaye ni balozi wa kampeni hii ya Kilimo Inalipa, Jikite, akisisitiza kwamba kilimo ndio Mkombozi wa Taifa letu la Tanzania

Wadau mbalimbali wa kilimo, wakikubali kwamba sekta ya kilimo inalipa!

Dhamira yetu, nia yetu ni kufanya Tanzania iweze kupata maendeleo kwa kupitia kilimo.

Tunaamini kilimo ndio uti wa mgongo wa Tanzania, kilimo ndio mkombozi pekee wa ajira kwa vijana Tanzania na watu wote. Lakini kilimo ndio ya maendeleo ya msingi kwa ajili taifa letu tukufu la Tanzania.

Sasa nafurahia kuona ANSAF pamoja na ONE wameamua kua na sisi. Nataka kuwaambie kwamba, kuna mmoja kati ya wachangia hoja hapa amesema vijana wanakimbia kijijini kwenda mjini lakini ajira zipo kulekule kijijini.

Tuna ardhi nzuri yenye rutuba na tumebarikiwa kuwa na nafasi, nyie mnaweza mkashiriki kwa kuona sasa hivi Iringa mvua zinanyesha.Tuna ardhi iliyotukuka sana, tuigeuze na tuamue  kufanya kilimo kama mkombozi wa Tanzania.

"Nafurahi sana, najiona nimebalikiwa sana sana kua part and parcel kwenye kampeni hii ya kufanya kilimo kuwa mkombozi kweli wa Mtanzania", alisema Profesa J.


Dokii, Profesa J na Mrisho Mpoto wakifatilia mjadala kwa makini

Wadau mbalimbali wa kilimowakisikiliza kwa makini
 Profesa J (Katikati) akielezea ujuzi wake katika sekta ya Kilimo, Kulia ni Mrisho Mpoto na kushoto ni Masoud Kipanya-mabalozi wa kampeni hii ya Kilimo Inalipa, JIKITE!



Wednesday 19 March 2014

Mrisho Mpoto: "Kilimo tusikiweke kwenye mengineyo"

   Kilimo kinalipa! 

"Neno “Haiwezekani” tuliondoe kwenye akili zetu. Mambo yanawezeka,

Mpoto, akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma, wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Kilimo wa Afrika na Kampeni ya Kilimo Inalipa, Jikite.

Mjomba akizungumza na wakulima wakati wa uzinduzi wa Mwaka wa Kilimo wa Afrika na Kampeni ya Kilimo Inalipa, Jikite, Kijijini Kaning'ombe Mkoani Iringa.













"Neno kilimo tusiliweke kwenye mengineyo", tukiliweka kwenye menginenyo tutakua tunazungumza tu na mambo hayatakuja kutokea. 

Mimi na mabalozi wenzangu tunatamka kwamba Mwaka huu wa Kilimo wa Afrika utakua wenye mafanikio chanya." Alisema Mpoto wakati wa uzinduzi wa kamepeni ya Kilimo Inalipa, Jikite huku hamasa kubwa ikitolewa zaidi kwa vijana      kujikita kwenye kilimo biashara .
                    Takwimu, Taarifa Tumekwishazisikia, Tujikite!!!


Mwakilishi kutoka ONE, Mercy Erhiawarien
Mkurugenzi Mtendaji wa ANSAF, Audax Rukonge
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk.Christine Ishengoma akiwa na Mkulima

wadau mbalimbali wa kilimo nao walishiriki uzinduzi huu

Thursday 13 March 2014

KATIKA KUAZIMISHA MWAKA WA KILIMO WA AFRIKA, ANSAF YAZINDUA KAMPENI YA KILIMO INALIPA, JIKITE.





                     Mkurugenzi Mtendaji wa ANSAF, Audax Rukonge

Jukwaa la Wadau wa Kilimo (ANSAF), limezinduzi wa Mwaka wa Kilimo barani Afrika, uliotangazwa 2012 na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) Rais Thomas Yayi Boni. Kwa Tanzania Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha Kaning'ombe Mkoani Iringa.
"kwa muda mrefu sasa jamii imekua ikiamini na kutafsiri kilimo kwa mtazamo hasi, hivyo kushindwa kuzitambua fursa zinazotokana na sekta hio".Bwana Rukonge aliyasema hayo  na kuitaka jamii iachane na kasumba ya kuona sekta ya kilimo kuwa ni ya watu walioshindwa kufanikiwa katika maisha, wazee ama wastaafu katika utumishi wa umma. Badala yake wametakiwa kutambua umuhimu wa kilimo katika kutoa fursa zinazochangia ukuaji wa uchumi na kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira nchini.


Nae mwakilishi wa taasisi ya ONE kutoka Afrika Kusinu Mercy Erhiawarien alisema nchi za Afrika zinapaswa kutekeleza Azimio la Maputo kwa Mwaka 2003 kuhusu kilimo. Kati ya nchi 53 ni nchi nane zimefanikiwa kutekeleza azamio hio, Kampeni ya ‘Kilimo Inalipa, Jikite’ inalenga kuwahamasisha watoa maamuzi, watunga sera na wadau wa kilimo kubadilisha kilimo huku fursa zaidi zikitolewa kwa wanawake na vijana.


Kwa upande wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Iringa  Dk. Christine Ishengoma aliwaasa wakulima kutumia kwa usahihi mbolea za kukuzia mazao, huku akithibitisha kwamba serikali katika ngazi tofauti inazifanyia kazi changamoto zinzowakabili wakulima kuhusu pembejeo.



Uzinduzi wa Mwaka wa kilimo pamoja na kampeni ya Kilimo Inalipa, Jikite ilipambwa na vikundi vya ngoma